Jumapili 28 Septemba 2025 - 07:59
Wajibu wetu ni kutekeleza majukumu na kupambana na adui

Hawza/ Sheikh Hassan Abdullah alisema: “Wapo baadhi ya watu leo wanaodhani kwamba tumeshindwa, sisi katu hatujashindwa, kushindwa ni pale tu ambapo adui anafanikisha malengo yake.”

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha  Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Hassan Abdullah, Mwenyekiti wa Bodi ya Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu Lebanon, alipokutana na ujumbe wa wanafunzi kutoka Shule za al-Imam al-Mahdi (aj), alisema:
“Tulipigana mapambano mengi na adui Wazayuni, wakati mwingine tulishinda, na wakati mwingine hatukushinda, wakati mwingine vijana walifanya oparesheni iliyofanikiwa kwa asilimia 100, na mara nyingine zilishindwa kwa asilimia 100, lakini kushindwa hakukutulazimisha kusalimu amri, bali kulitulazimisha kuchunguza sababu zilizosababisha kushindwa huko, ili katika oparesheni zijazo tuzizingatie na kuhakikisha uwezo wa mapambano hayo.”

Sheikh Abdullah akaongeza kusema: “Wapo wanaodhani leo kuwa tumeshindwa, lakini sisi katu hatujashindwa, kushindwa ni pale tu ambapo adui anafanikisha malengo yake.”

Mjumbe mwandamizi wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu aliendelea kusema: “Dhima halisi ya ushindi wa adui ni kwamba adui anapofanikisha malengo yake dhidi yako, hapo ndipo ameshinda, lakini upande wenu, endapo mtafanya jambo linalomzuia adui kufanikisha malengo yake, bila kujali hasara mlizopata, basi mmemshinda yeye.”

Sheikh Abdullah akabainisha: “Hoja si kwamba ni watu wangapi wameuawa mashahidi, au nyumba ngapi zimebomolewa, au watu wangapi wamejeruhiwa, bali hoja ni iwapo adui Mzayuni amefanikisha lengo lake au la  lengo kuu la adui Mzayuni katika vita hivi ni kuiangamiza Hizbullah, ikiwa tutaibuka washindi, basi licha ya kujitolea mhanga kwa kiwango kikubwa, adui hatoweza kulifikia lengo lake, hata kama Sayyid Hassan Nasrullah na Sayyid Hashim Safiuddin wameuawa kishahidi, hiyo pekee haitufanyi tushindwe.”

Akaendelea kusema: “Tulazimike daima kuzingatia kwamba sisi hatukukalifishwa na ushindi, Mwenyezi Mungu hakututakasa na kutuwajibisha ushindi, bali ametuwajibisha kufanya juhudi na kupambana, wakati mwingine, katika kutekeleza jukumu hilo, tunafanikisha malengo na kushinda kikamilifu, na wakati mwingine sivyo.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha